(Chorus)
Kila kitu nachofanya unaona hakifai baby gal, mimi nifanyeje?
Nimefanya mambo mengi nikuridhishe wee lakini gal, You driving me crazy
Nifanye kitu gani uelewe!
Nifanye jambo gani uridhike!
Baby gal (rough voc)
(Verse 1)
Nilihitaji unionyeshe mapenzi, Ooh ulinionyesha
Sikuhitaji unifanyie upuuzi, Ooh ungenikondesha
Nilikupa chochote ulichotaka, mradi nisione unahangaika
Lakini bado ulinifanyia pupa, tamaa kichwani zilikuzunguka
Nilihisi labda umenichoka, kumbe tamaa tu zinakuhangaisha
Nionyeshe mapenzi na huba, hivyo vyote mpenzi vinapita x2
(Chorus x2)
(Verse 2)
Ulimtamani mwenye simu mkononi, Ooh nami nikanunua
Ulimtamani mwenye dreads kichwani, Ooh kama nywele nikafuga
Ulinifanya nisifiwe njiani, eti kwa kuwa mii najithamini
Ila ukweli wangu upo moyoni, upendo wangu kwako niliuamini
Kama gari, fedha, nyumba nilikupa
Lakini bado penzi letu liliyumba
Ulitamani vingine vilivyo bomba, Oh uwo uwo navyo ulipata
(Chorus x2)
(Bridge)
Napenda kukuona ukifurahi lakini jua tamaa haifai
Sasa nataka, unieleze unachotaka
Sio unione, mimi kama takataka
Kila nachofanya, kukiona kama taka
Utani force kamba yetu kuikata
Wakati muda, bado haujawadia
Baby gal baby gal, Hey iyeah iyeah
(Chorus x2)
END!
# | Top 3 Mad Ice |
---|---|
1 | Mad Ice - Wange |
2 | Mad Ice - Malaika |
3 | Mad Ice - Nionyeshe Njia |